Psalms 102

Maombi Ya Mtu Mwenye Taabu

(Maombi Ya Mtu Aliyechoka. Anapoteseka, Anapomimina Malalamiko Yake Kwa Bwana)


1 aEe Bwana, usikie maombi yangu,
kilio changu cha kuomba msaada kikufikie.

2 bUsinifiche uso wako
ninapokuwa katika shida.
Unitegee sikio lako,
ninapoita, unijibu kwa upesi.


3 Kwa kuwa siku zangu zinatoweka kama moshi,
mifupa yangu inaungua kama kaa la moto.

4 cMoyo wangu umefifia na kunyauka kama jani,
ninasahau kula chakula changu.

5 dKwa sababu ya kusononeka kwangu kwa uchungu,
nimebakia ngozi na mifupa.

6 eNimekuwa kama bundi wa jangwani,
kama bundi kwenye magofu.

7 fNilalapo sipati usingizi,
nimekuwa kama ndege mpweke
kwenye paa la nyumba.

8 gMchana kutwa adui zangu hunidhihaki,
wale wanaonizunguka hutumia jina langu kama laana.

9 hNinakula majivu kama chakula changu
na nimechanganya kinywaji changu na machozi

10 ikwa sababu ya ghadhabu yako kuu,
kwa maana umeniinua na kunitupa kando.

11 jSiku zangu ni kama kivuli cha jioni,
ninanyauka kama jani.


12 kLakini wewe, Ee Bwana, umeketi katika kiti chako cha enzi milele,
sifa zako za ukuu zaendelea vizazi vyote.

13 lUtainuka na kuihurumia Sayuni,
kwa maana ni wakati wa kumwonyesha wema;
wakati uliokubalika umewadia.

14 mKwa maana mawe yake ni ya thamani kwa watumishi wako,
vumbi lake lenyewe hulionea huruma.

15 nMataifa wataogopa jina la Bwana,
wafalme wote wa dunia watauheshimu utukufu wako.

16 oKwa maana Bwana ataijenga tena Sayuni
na kutokea katika utukufu wake.

17 pAtaitikia maombi ya mtu mkiwa,
wala hatadharau hoja yao.


18 qHili na liandikwe kwa ajili ya kizazi kijacho,
ili taifa litakaloumbwa baadaye waweze kumsifu Bwana:

19 rBwana alitazama chini kutoka patakatifu pake palipo juu,
kutoka mbinguni alitazama dunia,

20 skusikiliza vilio vya uchungu vya wafungwa
na kuwaweka huru wale waliohukumiwa kufa.”

21 tKwa hiyo jina la Bwana latangazwa huko Sayuni
na sifa zake katika Yerusalemu,

22 uwakati mataifa na falme zitakapokusanyika
ili kumwabudu Bwana.


23 vKatika kuishi kwangu alivunja nguvu zangu,
akafupisha siku zangu.

24 wNdipo niliposema:
“Ee Mungu wangu, usinichukue katikati ya siku zangu;
miaka yako inaendelea vizazi vyote.

25 xHapo mwanzo uliweka misingi ya dunia,
nazo mbingu ni kazi ya mikono yako.

26 yHizi zitatoweka, lakini wewe utadumu,
zote zitachakaa kama vazi.
Utazibadilisha kama nguo
nazo zitaondoshwa.

27 zLakini wewe, U yeye yule,
nayo miaka yako haikomi kamwe.

28 aaWatoto wa watumishi wako wataishi mbele zako;
wazao wao wataimarishwa mbele zako.”
Copyright information for SwhKC